Namna ya kumkaribia Mungu

Kwa Muda mrefu nimekuwa nafikiri ni kwa jinsi gani naweza kuwa karibu na uwepo wa Mungu kila wakati. Watu wengi tunapata shida hasa linapokuja Suala la kukaa  katika uwepo wa Mungu. Utakuta muumini akienda eneo la ibada anajazwa na uwepo wa Mungu lakini kitendo cha kutoka eneo lile ibilisi anaiteka akili yake na kumfunga tena minyororo.
Mpendwa msomaji,maandiko katika kitabu cha Yakobo 4:8.yanatwambia mkaribieni Mungu naye atawakaribia,kwahiyo unaweza kuona ni kwa jinsi gani tunao wajibu wa kumtafuta kwa bidii huyu Mungu tunayemtumainia
Napenda kwa kifupi Kabisa nikueleze ni kwa namna gani Utaweza kudumu  katika uwepo wa Mungu.
Kwanza, jifunze kuisikia sauti ya Mungu. Hili nalo ni somo ambalo linahitaji ufafanuzi wa Kina; Mungu husema nasi  kwa jinsi za tofauti cha msingi ni kuweza kupambanua kwamba sauti hii ninayoisikia ni ya Mungu au ya shetani?
Jifunze kutii sauti ya Mungu maana utaweza kuepuka na mitego ya kishetani na malaika sake wachafu.
Muite Mungu wakati wote na katika mipango yako yote ifanye kwa utukufu wake. Hapa namaanisha maombi yasikome moyoni mwako. Biblia inapotwambia kesheni msingi ni kwamba tudumu Siku zote katika kumtegemea Mungu. Barikiwa sana
Itaendelea......

Comments